DILI:Xanana Gusmao apendekeza serikali ya muungano | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DILI:Xanana Gusmao apendekeza serikali ya muungano

Kiongozi wa East Timor Xanana Gusmao anapendekeza kuundwa kwa serikali ya muungano ya vyama vinne bila kukihusisha chama kilichopata ushindi katika uchaguzi wa wabunge mwaishoni mwa juma lililopita.Muungano huo unaongozwa na chama chake cha National Congress for the Reconstruction of East Timor unawasilisha matokeo rasmi kwa Rais Jose Ramos-Horta kuidhinishwa.

Bwana Gusmao ambaye ni rais wa zamani wa nchi hiyo anaheshimika kwa nafasi aliyochukua wakati wa kujikomboa kwa Timor ya Mashariki baaada ya kutawaliwa na Indonesia kwa miaka 24.Hata hivyo kiongozi huyo hajatangaza rasmi iwapo atakubali nafasi ya Waziri Mkuu endapo ombi hilo litakubaliwa.

Muungano huo unawakilisha viti vingi zaidi katika bunge lililo na nafasi 65 japo haujumlishi chama tawala cha Fretilin kilichopata asilimia 29 ya kura zote katika uchaguzi wa jumamosi iliyopita.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com