1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DILI: Wagombea wanane washindwa kupata asilmia 50

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAi

Uchaguzi wa urais wa Timor Mashariki utarudiwa tena mapema mwezi ujao baada ya wagombea wote wanane kushindwa kufikia kiwango cha asilimia 50 kilicho hitajika.

Tume ya uchaguzi ya Timor Mashariki imesema kwamba Lu-Olo Guterres mgombea wa chama kinachotawala anaongoza kwa silimia 29 dhidi ya waziri mkuu Jose Ramos-Horta ambae ana asilimia 22 kufuatia asilimia 70 ya kura zilizohesabiwa hadi kufikia sasa.

Matokeo rasmi yatatangazwa baada ya siku kadhaa.