1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dili. Mshindi wa tuzo ya Nobel ashinda kwa kishindo.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3E

Mshindi wa tuzo ya Nobel ya amani Jose Ramos – Horta ametoa ahadi ya kuondoa mvutano mkubwa wa kisiasa katika Timor ya mashariki baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi wa rais.

Australia na New Zealand , nchi jirani ambazo zina wanajeshi wao wa kulinda amani nchini humo, wamempongeza kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 57 kwa ushindi, ambao wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa ulikuwa wa amani na wa haki.

Matokeo rasmi yanampa Ramos – Horta asilimia 75 ya kura zilizopigwa siku ya Jumatano, ikiwa asilimia 90 ya kura zimekwisha hesabiwa.

Mpinzani wake katika uchaguzi wa duru ya pili Francisco Guterres , kiongozi wa chama cha mrengo wa shoto nchini humo cha Fretilin , bado hajakubali kushindwa, lakini kundi lake la kampeni limesema kuwa atakubali matokeo hayo.