Didier Drogba kulishtaki gazeti la Daily Mail | Michezo | DW | 15.04.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Didier Drogba kulishtaki gazeti la Daily Mail

Nyota Didier Drogba amesema atachukua hatua ya kiesheria kuhusiana na tuhuma kuwa shirika lake la hisani limetumia chini ya asilimia moja ya fedha zilizochangishwa kwa ajili ya miradi muhimu

Gazeti maarufu la Uingereza la Daily Mail lilisema kuwa pauni 14,000 tu kati ya pauni milioni 1.7 zilizotolewa na wahisani kwa wakfu wa Didier Drogba zimetumika kuwanufaisha watoto nyumbani kwao Cote d'Ivoire.

Tume ya inayoshughulika na mambo ya hisani nchini Uingereza imesema inachunguza shughuli za wakfu huo ulioanzishwa mwaka wa 2009 na aliyekuwa mchezaji huyo wa Chelsea.

Drogba mwenye umri wa miaka 38, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Ligi Kuu ya Kandanda ya Canada, amekanusha tuhuma hizo katika taarifa yenye maneno mazito ambayo amesema habari hizo za Daily Mail ni za kumchafulia jina.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Yusuf Saumu