DIANI KENYA.Hali ya usalama yazua hofu na wasomali wawili wasakwa | Habari za Ulimwengu | DW | 20.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DIANI KENYA.Hali ya usalama yazua hofu na wasomali wawili wasakwa

Mtu mmoja ameuwawa na polisi katika uvamizi dhidi ya kambi ya kutoa mafunzo kwa magenge ya kihalifu yanayolenga kufanya mashambulizi kwenye eneo la pwani nchini Kenya kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Hali imekuwa ya kutia wasiwasi katika taifa hilo la afrika mashariki katika kipindi cha miezi kadhaa sasa huku wadadisi wengi wakihofia hali hiyo inachochewa kisiasa.

Wakati huo huo polisi nchini humo imesema inawasaka watu wawili wenye asili ya kisomali wanaoshukiwa kuhusika moja kwa moja na mripuko wabomu lilitokea wiki iliyopita mjini Nairobi ambapo mtu mmoja aliuwawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com