1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DHAKA: Mgomo mkuu wa upinzani umesitisha huduma

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCta

Mgomo mkuu umesimamisha huduma zote katika mji mkuu wa Bangladesh Dhaka.Shule na ofisi zimefungwa ingawa kwa kawaida katika nchi hiyo ya kiislamu jumapili ni siku ya kufanya kazi. Wapinzani wanataka mabadiliko yafanywe katika mfumo wa uchaguzi na vile vile wakuu wa halmashauri ya uchaguzi wafukuzwe kazi.Wakuu hao wametuhumiwa kuwa wamefanya udanganyifu.