Dereva Rosberg ashinda Austrian Grand Prix | Michezo | DW | 22.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dereva Rosberg ashinda Austrian Grand Prix

Baada ya kumpiku mpinzani wake katika timu ya Mercedes Lewis Hamilton katika mashindano matatu kati ya manne yaliyopita, dereva Nico Rosberg ana matumaini kuwa amepata kiungo muhimu kilichokuwa kikikosekana

Dereva Nico Rosberg anasema ushindi wa Austrian Grand Prix umempa kiungo muhimu kiliichokosekana kushinda taji la Formula One mwaka huu: ukakavu zaidi.

Rosberg, aliyemaliza makamu bingwa mwaka jana nyuma ya Hamilton, sasa yuko nyuma ya mpinzani wake huyo wa Mercedes na pengo la pointi kumi baada ya ushindi wa kuridhisha wa mkondo wa Asutrian Grand Prix hapo jana. Hii ni baada ya kutumia ujuzi mkubwa kumpiku Hamilton katika kona ya kwanza ya mashindano hayo.

Hamilton ameshinda mashindano matano dhidi ya matatu ya Rosberg kufikia sasa msimu huu. Felipe Massa wa timu ya Williams alimaliza wa tatu mbele ya nambari nne Sebastian Vettel wa kikosi cha Ferrari.

Mwandishi: Bruce Amani
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman