1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UEFA Chapions League | Ferencvaros vs FC Barcelon | Dembele
Picha: Bernadett Szabo/REUTERS

Dembele ang'aa mno La Liga

24 Oktoba 2022

Barcelona hapo Jumapili walipata ushindi wa kuridhisha wa 4-0 walipochuana na Athletic Bilbao katika uwanja wao wa nyumbani wa Camp Nou.

https://p.dw.com/p/4Id08

Lakini aliyezungumziwa mno katika mpambano huo ni winga wao raia wa Ufaransa Ousmane Dembele ambaye licha ya kufunga goli, aliwaandalia pasi wachezaji wenzake, Robert Lewandowski, Ferran Torres na Sergi Roberto.

Na wapinzani wao ambao ni vinara Real Madrid waliwazidi nguvu Sevilla 3-1 na kocha wao Carlo Ancelotti amewaambia wachezaji wake wanastahili kuendelea kupambana licha ya msururu wa mechi zinazokuja.

"Na tuko sawa, kikosi kiko sawa. Ni wakati katika msimu ambapo hatustahili kuangalia mbele sana, tunastahili kuwa makini kwasababu hizi mechi zinakumaliza nguvu kimwili na kisaikolojia. Hatuwezi kusita, ni sharti tuendelee na tujitese uwanjani na kujaribu kushinda mechi," alisema Ancelotti.