1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Real Sociedad yampiga kalamu kocha David Moyes

10 Novemba 2015

David Moyes amepigwa kalamu kama kocha wa Real Sociedad ya Uhispania, siku moja kabla ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu ajiunge na klabu hiyo. Eusebio Sacristan amechukua nafasi yake

https://p.dw.com/p/1H2cy
David Moyes Porträt
Picha: Reuters

Mkufunzi huyo wa umri wa miaka 52 aliongoza klabu hiyo kumaliza nambari 12 msimu uliopita baada ya kuchukua usukani manmo Novemba 10, 2014.

Real Sociedad iko karibu sana na eneo la kushushwa ngazi, ikiwa juu kutokana na wingi wa mabao baada ya kulazwa 2-0 Ijumaa ugenini na klabu iliyopandishwa ngazi msimu huu Las Palmas. Hiyo ni mechi yao ya nne kushindwa katika mechi tano katika La liga. Moyes alijiunga na Sociedad baada ya kufutwa kazi katika klabu ya Ligi Kuu ya Kandada ya England, Manchester United

Taarifa kutoka kwa Sociedad imesema klabu hiyo imeamua kukatiza mkataba wa Moyes. Kocha wa zamani wa Celta Vigo na BARCELONA B Eusebio Sacristan mwenye umri wa miaka 51 amechukua usukani na ataiongoza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu.

Klabu hiyo kwa sasa imo nambari 16 ligini na itakutana na washindi wa Europa League Sevilla na mabingwa wa Ulaya Barcelona mechi mbili zijazo La Liga baada ya mapumziko ya kimataifa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Sekione Kitojo