DAMASCUS: Waziri Mkuu wa Irak asema ziara yake nchini Syria ni ya manufaa | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 22.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

DAMASCUS: Waziri Mkuu wa Irak asema ziara yake nchini Syria ni ya manufaa

Waziri mkuu wa Irak bwana Nuri al-Maliki amesema kuwa Syria ipo tayari kusaidia katika juhudi za kuleta utengemavu nchini Irak.

Bwana al-Maliki amesema hayo kwa wandishi habari mjini Damascus baada ya mazungumzo yake na rais Bashar al-Assad wa Syria .

Waziri Mkuu huyo wa Irak, yupo nchini Syria kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu, anayoifanya kwa mara ya kwanza tokea awe waziri mkuu wa Irak.

Bwana al –Maliki amesema nchi yake na Syria zina maslahi ya pamoja na zinapaswa kutatua matatizo kwa pamoja kwa manufaa yao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com