1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Syria yakosoa juhudi za kupatikana amani kati yake na Israil.

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3T

Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema jitihada za kutafuta amani kati ya serikali yake na Israil hazijafanikiwa vyovyote ingawa kumekuwa na juhudi za kimataifa kujaribu kuyapatanisha mataifa hayo mawili.

Bashar aliwaambia wabunge wa nchi yake Marekani imekuwa ikiishinikiza Israil idumishe uadui kati yake na Syria.

Rais huyo wa Syria amesema washika dau wote wanapaswa kuzingatia suala la ardhi kwa ajili ya amani na Israil iwe tayari kurejesha ardhi zote za mataifa ya kiarabu.

Bashar al-Assad amesema iwe iwavyo ni lazima Syria irejeshewe eneo la milima ya Golan.

Syria imekuwa mara kwa mara ikitolea wito Israil kushauriana nayo kuhusu kurejeshwa eneo la milima ya Golan lililotekwa na Israil mwaka 1967.