1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS : Syria kutoshirikana na mahkama ya kimataifa

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpT

Serikali ya Syria inadokeza kwamba huenda isitowe ushirikiano wake kwa mahakama ya kimataifa inayopangwa kuundwa kuchunguza mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.

Katika baruwa kwa Umoja wa Mataifa serikali ya Syria imesema kwa vile haikushauriwa juu ya kuundwa kwa mahkama hiyo haki ya kujiamuliwa mambo yake yenyewe ya mataifa fulani pamoja na raia wake inaweza kukiukwa.

Uchunguzi unaoendelea hivi sasa umewahusisha maafisa waandamizi wa usalama wa Syria na Lebanon na mauaji ya Hariri na watu wengine 22 hapo mwezi wa Februari mwaka 2005.

Baraza la mawaziri la Lebanon linatarajiwa kukutana leo hii kuidhinisha uundaji wa mahkama hiyo ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni siku mbili baada ya maziko ya waziri wa serikali ya Lebanon Piere Gemayel ambaye alipigwa risasi na kuuwawa mjini Beirut hapo Ijumanne.