DAMASCUS : Rais Talabani wa Iraq ziarani Syria | Habari za Ulimwengu | DW | 15.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DAMASCUS : Rais Talabani wa Iraq ziarani Syria

Rais Jalal Talabani wa Iraq amewasili Damascus kwa mazungumzo na Rais Bashar al Assad juu ya njia za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kukomesha umwagaji damu unaoendelea nchini Iraq.

Assad amemkaribisha Talabani katika hafla maalum kwenye kasri la rais.Ziara ya Talabani ya siku sita nchini Syria ni ya kwanza kuwahi kufanywa na Rais wa Iraq tokea nchi hizo mbili zivunje uhusiano wake wa kibalozi hapo mwaka 1980.Syria na Iraq zilirudisha uhusiano wao wa kibalozi mwezi Novemba mwaka jana.

Marekani na Iraq zimekuwa zikiishutumu Syria kwa kushindwa kuchukuwa hatua ya kuwazuwiya wanamgambo kujipenyeza nchini Iraq kutokea Syria madai ambayo serikali ya Syria imeyakanusha mara kadhaa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com