1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damascus. Pelosi anamatumaini ya kupata amani mashariki ya kati.

5 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCN

Spika wa baraza la wawakilishi nchini Marekani Nancy Pelosi, amesema kuwa rais wa Syria Bashar al – Assad amemwambia kuwa serikali yake iko tayari kuanza majadiliano ya amani na Israel. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Damascus , Pelosi amesema kuwa amempatia ujumbe kama huo rais Assad kutoka kwa waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert.

Amesema ametumia mkutano huo kueleza wasi wasi wa Marekani juu ya wapiganaji wanaotoka Syria na kufanya mashambulizi katika ardhi ya Iraq, pamoja na uungaji mkono wa Syria kwa makundi ya wapiganaji ya Hamas na Hezboullah.

Pelosi anatarajiwa kukutana na baraza la ushauri la Saudi Arabia leo baada ya kuwa na majadiliano na mfalme Abdullah jana , kuhusiana na suala la Iraq katika sehemu ya mwisho ya ziara yake yenye utata katika mashariki ya kati.

Rais George W. Bush ameikosoa vikali ziara ya Pelosi nchini Syria, akisema kuwa inatoa ujumbe ambao si sahihi kwa Syria.