1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dalai Lama atishia kujiuzulu

Kalyango Siraj18 Machi 2008

Pia amekanusha kuchochea ghasia Tibet

https://p.dw.com/p/DQlx
Kiongozi wa Kiroho wa Tibet Dalai Lama wakati wa mkutano na waandishi habari.Ametishia kujiuzulu ikiwa ghasia zitaendelea TibetPicha: AP

Kiongozi wa kidini wa Kibudhaa kutoka Tibet,Dalai Lama amesema kuwa yuko tayari kujiuzulu wadhifa wake ikiwa hali itaendelea kuwa mbaya katika eneo lake anakotoka,huku akikanusha madai ya serikali ya China kuwa anachochea ghasia katika eneo hilo.

Tisho la kujiuzulu kwa Dalai Lama ikiwa machafuko hayatakoma katika jimbo la Tibet amelitoa leo mbele ya wandishi habari akiwa katika makao yake ya uhamishoni ya Dharamsala, kaskazini mwa nchini India.

Matamshi ya Dalai Lama yanafuata kauli ya waziri mkuu wa China-Wen Jiabao,ambapo alimulaumu Lama kwa kuchochea ghasia katika mkoa huo kwa lengo la kuhujumu michezo ya Olimpiki ambayo itafanyika Beijing kuazia mwezi Agosti mwaka huu.

Serikali ya China inasema Dalai Lama ndie anachochea ghasia sasa za Tibet akiwa na nia ya kutafuta kuungwa mkono nia yake ya kutaka jimbo hilo kujitenga kutoka China,hasa akitumia wakati huu ambapo michezo ya Olimpiki ikiwa inakaribia.

Dalai Lama akikanusha hayo amesema kuwa yeye anapinga yeye anapinga ghasia za aina yote ziwe zinafanywa na wachina ama watibet, na kuongeza kuwa hana kinyongo na wachina wanachopigania ni kupewa uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Waziri mkuu wa serikali ya uhamishoni ya Dalai Lama,Samdhong Pimoche, alipoulizwa na waandishi habari kufafanua kile alichukuwa anamaanisha Dalai Lama kuhusu kujiuzulu,ameeleza kuwa hata akijiuzulu lakini atabaki kama Dalai Lama lakini sio kiongozi wa watu wake.

Matamshi ya kujiuzulu kwa Dalai Lama yamewashangaza baadhi ya wabunge wa bunge la uhamishoni.

Mbunge mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters kwa simu kutoka New Delhi India kuwa watu wa Tibet,wa ndani na nje, hawawezi kukubali Baba wao mtakatifu kujiuzulu.Ameongeza kuwa labda hiyo ndio njia yake mojawapo ya kuwapa wajumbe watu wake wa Tibet kuwa ikiwa maandamano yao yanaambatana na ghasia wayaepuke.

Maandamano yaliyoongozwa na watawa wa Kibudha ya mjini Lhasa mji mkuu wa jimbo la Tibet, ndio yaliyokuwa makubwa sana kuwahi kufanywa katika eneo hilo kwa kipindi cha takriban miongo miwili.

Maandamano hayo Ijumaa iliopita yalibadilika na kuwa ghasia ambapo,inadaiwa kuwa watu 80 ndio waliuawa.Lakini serikali ya kikomunisti ambayo inaontawala jimbo hilo tangu mwaka wa 1950 imekanusha hayo huku ikijaribu kutakasa jina lake hasa wakati michezo ya Olimpiki inapokaribia.

Takriban waTibet 2000 wamekusanyika leo kaskazini mwa India wakitaka umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi kuhusu madai ya kuwa china iliwauwa waandamanji katika mji wa Lhasa Tibeti.Pia kuna madai kuwa watu waliouliwa idadi yao imepanda kutoka 80 hadi 99.