DÜSSELDORF: Kanada yataka vifaru vya Kijerumani nchini Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 24.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DÜSSELDORF: Kanada yataka vifaru vya Kijerumani nchini Afghanistan

Vifaru vya kisasa vya jeshi la Ujerumani,huenda vikapelekwa kusini mwa Afghanistan hivi karibuni. Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Kijerumani “Rheinische Post“ serikali ya Ujerumani huenda ikakubali ombi la serikali ya Kanada kupeleka vifaru chapa ya “Chui“ vilivyo na kinga imara dhidi ya mabomu yaliotegwa ardhini.Kanada,imeomba vifaru hivyo kuwalinda wanajeshi wake walio nchini Afghanistan,chini ya uongozi wa NATO kama sehemu ya vikosi vya kimataifa vinavyolinda usalama nchini humo ISAF.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com