1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DÜSSELDORF: Ajali ya ujenzi imeua watu 5

26 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ci

Wafanyakazi 5 wamepoteza maisha yao katika ajali ya ujenzi wa mitambo ya nishati katika mkoa wa North Rhine Westphalia nchini Ujerumani.Wengine 6 wamejeruhiwa vibaya baada ya sehemu ya bwela yenye uzito wa tani 100 kuchomoka na kuanguka chini.Kuanzia mwaka 2009,mitambo hiyo miwili inayojengwa Grevenbroich,karibu na Düsseldorf, inatazamiwa kuzalisha megawati 2,200 za nishati kwa kutumia makaa.