1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CUF yahitimisha kampeni za uchaguzi Zanzibar

Elizabeth Shoo22 Oktoba 2015

Chama cha Wananchi CUF kimerejelea kauli yake ya kutaka Mamlaka Kamili kwa Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanzania.

https://p.dw.com/p/1GsqL
CUF Seif Sharif Hamad
Picha: DW/M. Ghassani

Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar na ambacho pia ni mshirika mdogo kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ya visiwa hivyo, Chama cha Wananchi, CUF, kimehitimisha leo kampeni zake za urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Jumapili, huku mgombea wake wa urais akirejelea kauli mbiu yake ya Mamlaka Kamili kwa Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanzania, na pia kumtaka mshindani wake mkuu kwenye uchaguzi huo, Dk. Ali Mohamed Shein, kutoa tamko la kukubali matokeo ya uchaguzi kama yatakavyokuwa endapo upigaji kura utakuwa huru na wa haki.

Sikiliza ripoti ya Mohammed Khelef hapo chini.