1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CUF yafungulia polisi mashtaka Zanzibar

Sudi Mnette14 Julai 2016

Chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kimelifikisha mahakamani jeshi la polisi kwa madai ya kuwashikilia kinyume na taratibu maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa chama hicho, akiwemo waziri wa zamani.

https://p.dw.com/p/1JOig
Polisi Pemba
Picha: picture-alliance/dpa

[No title]

Bado kamatakamata inaendelea kuripotiwa visiwani Zanzibar, ikihusishwa na uhasama wa kisiasa uliozuka visiwani humo kutokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka 2015 na baadaye ule wa marudio wa Machi mwaka 2016. Chama kikuu cha upinzani visiwani humo, CUF, kimelifikisha mahakamani rasmi jeshi la polisi kwa madai ya kuwashikilia wafuasi wake na maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa chama hicho, akiwemo waziri mmoja wa zamani, kinyume na taratibu za nchi. DW imezungumza na wakili wa watuhumiwa, Is-haka Ismail Sharif, akiwa katika eneo la mahakama kuu mjini Unguja ambapo kesi hiyo ikiendelea.