1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CPJ yaitaka DRC kuwaachia huru wanahabari walio kizuizini

Admin.WagnerD25 Agosti 2022

Kamati ya kimataifa ya kuwalinda waandishi wa habari CPJ, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuta kesi zote dhidi ya waandishi wa habari wawili ambao wapo kizuizini kwa takriban miezi minane sasa.

https://p.dw.com/p/4G39f
Demonstrationen gegen die Präsidentschaftspartei Union für Demokratie und sozialen Fortschritt (UDPS) in Kinshasa
Picha: Getty Images/AFP/A. Mpiana

Serikali ya Kongo pia imetakiwa kutoweka vikwazo katika dhamana zao na kisha kuendelea kuwashikilia waandishi hao.

Waandishi hao walikamatwa mwezi Januari kwa tuhuma za kuhatarisha amani walipokuwa katika majukumu yao ya kazi. 

Patrick Lola  ni mwandishi wa kujitegemea na Christian Bofaya,  ni mwajiriwa wa kituo binafsi cha E Radio nchini humo, walikamatwa katika mji mkuu wa jimbo la Equateur, Mbandaka na shutumiwa kwamba wanahatarisha amani wakati wakiripoti juu ya maandamano mnamo Januari 10.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo mnamo Agosti 9 katika mahakama ya Cassation katika mji mkuu Kinshasa, waandishi hao wakiwa pamoja na waandaaji wa tatu wa maandamano hayo, walitakiwa kulipa kiasi cha dola ya marekani 1000 kwa kila mmoja sawa na faranga za kongo milioni 2.

Soma zaidi:Wafungwa watoroka gerezani DRC

Hata hivyo waandaaji wa maandamano hayo walifaulu kulipa kiasi hicho cha fedha na kuachiwa huru huku waandishi hao wawili wakishindwa kutekeleza masharit ya dhamana na kusalia kizuizini.

Mwanansheria anaewawakilisha mahakamani Jean-Claude Mafundisho ambae alizungumza na kamati ya kimataifa inayowalinda waandishi wa habari CPJ

"Masharti ya dhamana yamekuwa magumu kwa wanahabari hao."

CPJ waingilia kati kuhusisha mamalaka

Angela Quintal mratibu wa programa za Afrika katika kamati hiyo ya kimataifa ameiambia Dw Kiswahili kwamba hadi sasa wanaendelea kuihusisha amamalaka nchini humo ili kupata haki ya waandishi hao waliopo kizuizini kwa zaidi ya miazi minane.

Demokratische Republik Konog | Unruhen in Goma
Raia wa DRC wakiwa katika maandamano mjini GomaPicha: Guerchom NdeboAFP/Getty Images

Amewataja wandishi hao wawili ambao wamekuwa kizuizini kwa zaidi ya miezi nane kuwa wapo kizuizini bila ya sababu zaidi ni kuathiri kazi zao za kila siku.

Soma zaidi:Waliouawa kwenye maandamano DRC kuzikwa Ijumaa

Ameongeza kwamba wawili hao hawakua miongoni mwa waandamanaji bali walikuwa katika majukumu yao ya kila siku, kibaya zaidi walikamatwa wakiwa na waandaaji wa maandamano ambao ni wanasiasa.

 "Waandaaji wana fedha na wanamudu kulipa dola elfu 1000 na kuachiwa lakini waandishi wamesalia kizuizini sababu hawawezi kulipa dhamana" aliiambia DW

Wakili: wapewe dhamana au wahamishiwe Mbandaka

Wakili anaewakilisha waandishi hao ameiambia CPJ kwamba ni vema mahakama hiyo iwape waandishi hao dhamana.

Wakaazi Kivu washinikiza kuondolewa MONUSCO DRC

Ameongeza kuwa kama suala la dhamana litaendelea kusalia kuwa ni changamoto inawezekana kesi hiyo ihamishiwe katika mahakama ya mji wa Mbandaka kwa hatua zaidi ili haki ya wanahabari hao ipatikane.

Soma zaidi:UNICEF: Maelfu ya watoto hawana makaazi mashariki mwa DRC

Hata hivyo CPJ ilichukua hatua ya kuwaita wandaaji wa maandamano yaliosababisha waandishi hao kusalia kizuizini kwa kipindi chote, msemaji wa serikali ya Kongo na waziri wa mawasiliano Patrick Muyaya naibu mkuu wa wafanyakazi wa Wizara ya Sheria kwa majadiliano zaidi lakini jitihada hiyo haikuwa na mafanikio.