1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Corona: Mazingira ya wandishi wa habari hatarini

Ibrahim Swaibu
15 Mei 2020

Baadhi yao wamepoteza ajira, kupunguziwa mishahara na wengine kuandamwa na vyombo vya usalama

https://p.dw.com/p/3cH1x
Demonstration gegen ein Mediengesetzt in Nairobi
Picha: imago stock&people

Wakati janga la virusi vya Corona likizidi kuutikisa  ulimwengu na kukwamisha shughuli mbalimbai duniani, mazingira ya wandishi wa habari barani Afrika nayo yameathirika pakubwa, baadhi yao wamejikuta katika hali ya kuandamwa na vyombo vya usalama na wengine kupunguzwa mishara yao licha ya kuwa katika kipindi hiki kazi yao ni muhimu sana.

Katika hali ya kawaida kabla ya virusi hivyo kuingia, mshahara wa wandishi habari wa kituo cha radio cha Dandal Kura Kaskazini mwa Nigeria ulikuwa ni takribani dola 100 kwa kila mwezi.

Licha ya kwamba mshahara huo ni duni kuweza kujikimu kimaisha, kwa sasa umepunguzwa na zaidi ya theluthi ya wandishi  wa idhaa hiyo kusimamishwa kazi kwa muda. Amesema Faruku Dalhatu mkuu wa kituo hicho. Faruku ameimbia DW kuwa kwa sasa kituo hicho hakipokei  matangazo ya biashara hali ambayo imepunguza kipato chake.

''Sijapokea mshahara wkwa miezi sita sasa, amesema Oscar Mulbah mkrugenzi mkuu wa kituo cha redio cha Truth nchini Liberia na kuiambia DW kuwa hata kabla ya janga la Corona tasnai ya habari nchini mwake ilikuwa katika njia panda. 

Kadhalika nchini Libera , Helen Nah Sammie mkuu wa gazeti la Women Voices amesema wanaendesha  biashara hiyo kwa hasara kutokana na atahri za janga la Covid-19.

Nchini Niger amabapo pia kipato cha wandishi wa habari kimepungua, mhariri mkuu wa runinga ya Saraounia , Oumarou Gado anamatumaini kuwa kufuatia kulegeza kwa vizuizi vya kujikinga dhidi ya COVID-19, huenda tasnia hiyo ikaanza tena kuimarika.

Isitoshe, mbali kusababisha kupunguza mishahara, baadhi ya serikali zimelitumia janga la Corona ili kubinya uhuru wa wandishi wa habari licha ya kwamba huu ni wakati ambapo kazi yao ingehitajika zaidi.

Katika hotuba yake wiki iliopita katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa tahadhari kuwa huenda janga la Corona likakeugikia na kuwa janga la kibinadamu huku pia akitaka serikali duniani kulinda haki za wandishi wa habari.

Chanzo: DW