1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Conte aendelea kuiimarisha Chelsea

Sekione Kitojo
2 Novemba 2016

Katika ligi ya Uingereza PremieR League, Chelsea imeendelea kuchanja mbuga kuelekea juu kileleni mwa ligi  hiyo pamoja na timu tatu  za juu baada ya Jumapili kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton

https://p.dw.com/p/2S1Ck
UEFA EURO 2016 Achtelfinale Italien vs. Spanien Trainer Antonio Conte
Picha: picture-alliance/dpa/I. Langsdon

Eden Hazard  na  Diego Costa walifunga mabao hao na kukinyanyua kikosi cha Antonio Conte hadi katika nafasi ya nne, pointi  moja  nyuma  ya manchester  City, Arsenal na  Liverpool  ambazo  zina pointi  sawa  kilelele  na  kutenganishwa  na   wingi  tu  wa mabao.

Katika  La  Liga  timu  zinazocheza  katika  Europa  League Villareal, Athletic Bilbao  na  Celta  Vigo  zote  zilipata pigo Jumapili  katika  juhudi  zao  za  kujiunga  na  mbio za  kuwania  ubingwa  wa  Uhispania.

Villareal  iliangukia  pua  mbele  ya  Eibar  kwa  mabo  2-1 , Bilbao  iliridhika  na  sare  ya  bao 1-1 nyumbani  dhidi  ya mahasimu  wao  upande  wa  kaskazini  mwa  nchi  hiyo Osasuna  na  Celta  ilishikwa  shati  na  kutoka  sare  ya mabao 3-3  dhidi  ya  Las Palmas. Siku  ya  Jumamosi Barcelona  ilidonoa Granada  kwa  bao 1-0 , wakati  Alaves ilikandamizwa  kwa  mabao 4-1  dhidi  ya  Real Madrid, nayo Atletico  Madrid  ikaishindilia  Malaga  kwa  mabao 4-2.

Ligi  ya  Ulaya  inarejea  tena  uwanjani  kesho  Jumanne na  Jumatano, ambapo Manchester  City itakuwa nyumbani  ikiisubiri  Barcelona  baada  ya  kipigo  cha kudhalilisha  cha  mabao  4-0  katika  uwanja  wa  Camp Nou  katika  kundi  C  wiki  mbili  zilizopita. Manchester  City imepata  pointi  moja  tu  kutokana  na  michezo  yake miwili  ya  Champions League  iliyopita.

PSG inalenga kutinga hatua ya 16 za mwisho
PSG inalenga kutinga hatua ya 16 za mwishoPicha: Getty Image/AFP/F. Fife

Ushindi  wa  tatu mfululizo  wa  kikosi  cha  Barcelona kutoka  katika  jimbo  la  Catalan  unatkuwa  na  maana kwamba  watahitaji  sare  tu  katika  mchezo  unaofuatia kujihakikishia  tikiti  yao  katika  awamu  ya  mtoano. katika kundi  hilo Borussia  Moenchengladbach  inaikaribisha nyumbani  Celtic Glasgow , ambapo  katika  mchezo  wa kwanza  baina  ya  timu  hizo , Gladbach  ilipata  ushindi muhimu  wa  mabao 2-0  ugenini. Bayern Munich  ni  wageni  wa  PSV Eindhoven  na Atletico  Madrid  iko  nyumbani  ikiisubiri  Ristov  ya  Urusi katika  kundi  D.

Paris St. Germain  ina  miadi  na  basel  ya  Uswisi  na Arsenal  iko  nyumbani  kwa  Ludogorets Razgrad  ya Bulgaria  katika  mchezo  wa  kundi  A  ambalo linaoongozwa  na  Arsenal ikifuatiwa  na  PSG.

Mabingwa  wapya  wa  Champions League  barani  Afrika Mamelodi Sundowns walionya  kipigo  cha  mabao  2-1 jana  katika  ligi  ya  Afrika  kusini  dhidi  ya  Cape Town City  na  inabakia  mkiani  mwa  ligi  hiyo  siku  saba  baada ya  kutawazwa  mabingwa  wa  Afrika. Jua  kali , mipango ya  haraka  haraka  ya  mchezo  huo  na  sherehe  za baada  ya  ushindi  vilionekana  kuathiri  kwa  kiasi  kikubwa mmchezo  wa  mabingwa  hao  wa  Afrika  na  Cape Town City  wangeshinda  kwa  mabao  mengi  kutokana  na kutengeneza  nafasi  nyingi  za  mabao.

Mbio  za  magari.

Dereva Muingereza  Lewis Hamilton  ameshinda  mbio  za magari  za  Mexico Grand Prix  na  kuendeleza  mbinyo dhidi  ya  dereva  mwenzake  wa  magari  ya  Mercedes Nico  Rosberg  katika  mvio  za  Formula  one  zilizofanyika nchini  Mexico jana  Jumapili.

Na  kwa  taarifa  hiyo  nasema  sina  la  ziada  na nakutakia  jioni  njema , jina  langu  ni  Sekione  Kitojo , kwaherini.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae / afpe / rtre
Mhariri: Yusuf saumu