1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Colombo.Kuna uwezekano wa serikali kukubali mazungumzo ya amani na waasi.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1K

Kufuatia shambulio la kujitolea muhanga katika kituo cha wanamaji lililopelekea kuuwawa kwa mwanajeshi mmoja, jana usiku vikosi vya kijeshi vya serikali na waasi wa Kitamil, walishambuliana kwa risasi huko kaskazini mwa Sri Lanka, na kumjeruhi mwanajeshi mmoja.

Maafa hayo yamekuja kufuatia kuwasili kwa mjumbe wa Marekani Richard Boucher nchini Sri Lanka kwa ajili ya mazungumzo kati ya serikali na waasi.

Boucher katika ziara yake hiyo anategemewa kuhakikisha kwamba pande hizo mbili zinafikia makubaliano ya mazungumzo ya amani ambayo yamepangwa kufanyika mwezi huu.

Akizungumzia uwezekano wa kufanyika mazungumzo hayo kwa upande wa seriakli, afisa kutoka wizara ya Ulinzi ya Sri Lanka Keheliya Rambukwale alisema.

“Tunajukumu kwa Kaka zetu na dada zetu, kaka zetu wa Kitamil na dada zetu, ambako wanamalalamiko ya msingi, na masuala mengine kadhaa yanayohitaji kusuluhishwa“.