COLOMBO: Watu 40 wauwawa katika mapigano | Habari za Ulimwengu | DW | 21.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO: Watu 40 wauwawa katika mapigano

Watu takriban 40 wameuwawa katika mapigano ya hivi punde nchini Sri Lanka. Boti za jeshi la wanamaji ziliziharibu boti saba za waasi wa Tamil Tigers katika mapigano ya baharini hapo jana na kuwaua waasi wasiopungua 35.

Waasi wengine sita wameuwawa katika mapigano mengine yaliyozuka leo asubuhi kwenye ngome ya waasi wa Tamil Tigers huko Jaffna kaskazini mwa nchi hiyo.

Sri Lanka imekabiliwa na ongezeko kubwa la machafuko katika miezi michache iliyopita, hivyo kuzusha wasiwasi ikiwa kweli mazungumzo ya kutafuta amani kati ya serikali na waasi wa Tamil Tigers yaliyopangwa kufanyika mjini Geneva, Uswisii kati ya tarehe 28 na 29 mwezi huu, yatafaulu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com