1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Waasi wa Tamil Tigers waonya kupanua mapigano yao

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0S

Waasi wa Tamil Tigers leo wametishia kupanua mapigano yao dhidi ya majeshi ya serikali ya Sri Lanka, ikiwa serikali inataka vita. Onyo hilo limetolewa baada ya jeshi la wanamaji kutangaza limewaua waasi 20 wa Tamil Tigers.

Msemaji wa kundi hilo, Rasiah Ilanthirian, amesema waasi wako tayari kukubali vita au amani na wanasubiri hatua ya serikali kuhusiana na hali ya baadaye ya mogogoro huo.

Waasi sita waliuwawa leo asubuhi katika mapigano yaliyozuka kwenye ngome ya waasi wa Tamil Tigers huko Jaffna kaskazini mwa Sri Lanka.

Mazungumzo ya kutafuta amani kati ya serikali na waasi wa Tamil Tigers yamepangwa kufanyika mjini Geneva, Uswisi tarehe 28 na 29 mwezi huu.