COLOMBO: Vikosi vya serikali na Tamil Tigers wapambana upya | Habari za Ulimwengu | DW | 13.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO: Vikosi vya serikali na Tamil Tigers wapambana upya

Nchini Sri Lanka mapigano yamezidi kati ya vikosi vya serikali na waasi wa Tamil Tigers licha ya pande hizo mbili kukubali kuwa na majadiliano ya amani.Serikali mjini Colombo imesema,katika mapigano mapya yaliyozuka kwenye rasi ya Jaffna,wanajeshi 129 wameuawa na 500 wamejeruhiwa.Vile vile waasi 200 wameuawa.Lakini Tamil Tigers wamesema,wanamgambo wao 10 tu waliuawa katika mapigano hayo.Pande hizo mbili zinatazamia kukutana tarehe 28 Oktoba kwa majadiliano ya amani chini ya upatanishi wa Norway.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com