Colombo. Tamil Tigers washutumiwa kufanya shambulizi. | Habari za Ulimwengu | DW | 07.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Colombo. Tamil Tigers washutumiwa kufanya shambulizi.

Kiasi watu 11 wameuwawa na zaidi ya 40 wengine wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga katika basi kusini mwa Sri Lanka.

Mshambulizi huyo wa kujitoa muhanga anaaminika kuwa alikuwa mwanamke ambaye alibeba milipuko ndani ya basi hilo lililokuwa na watu wengi.

Shambulio hilo linafuatia shambulio lingine dhidi ya basi siku ya Ijumaa wakati abiria sita walipouwawa na wengine 70 kujeruhiwa karibu na mji wa Colombo.

Maafisa wanasema kuwa mashambulizi hayo yamefanywa na waasi wa Tamil Tigers, ambao wanapigana kupata taifa lao la Tamil. Tamil Tiger wamekana kuhusika na mlipuko huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com