COLOMBO: Tamil Tigers wafanya shamulizi lingine | Habari za Ulimwengu | DW | 27.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO: Tamil Tigers wafanya shamulizi lingine

Waasi wa kundi la Tamil Tigers wamefanya shambulizi lingine katika kambi ya kijeshi huko mashariki mwa Sri Lanka, ambapo trekta lililokuwa na mabomu limelipua kambi hiyo na kusababisha majeraha makubwa kwa askari waliyokuwepo.

Treka hilo lilibamizwa katika kambi hiyo ya Chenkaladi, huko mashariki mwa Sri Lanka ambapo majeshi ya serikali yamekuwa yakiendesha operesheni kabambe dhidi ya waasi hao wa Tamil Tigers.

Shambulizi hilo limekuja siku moja tu baada ya waasi hao wa Tamil Tigers kufanya shambulizi lao la kwanza la anga katika kambi ya jeshi la anga pembezoni mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sri Lanka ambapo wanajeshi watatu waliauawa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com