1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOMBO: Serikali na waasi nchini Sri-Lanka, tayari kwa mazungumzo

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1m

Serikali ya Sri-Lanka na waasi wa Tamil Tigers wamesema wako tayari kwa mazungumzo ya amani. Tamko hilo limetolewa siku moja baada ya kufanyika mauaji katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga ambapo watu 103 waliuawa na wengine 150 kujeruhiwa. Mazungumzo hayo yalipangwa kufanyika mjini Geneva nchini Usuisi tarehe 28 na 29 mwezi huu, lakini wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema hamna matumaini mazungumzo hayo kuzaa matunda kufuatia kuzidi kuathirika kwa hali ya usalama hata kabla ya mazungumzo yenyewe kuanza. Ngede za kivita za serikali ya Sri-lanka zilishambulia maeneo yanayodhibitiwa na waasi kaskazini mashariki mwa nchi katika mkesha wa shambulio la bomu lililowauwa watu zaidi ya 100, ambapo waasi wa Tamil Tigers walilaumiwa kuhusika. Serikali ilisema shambulio la ndege zake lililenga kituo cha waasi wa Tamil Tigers ambao kwa upande wao, wanasema ndege zililenga kijiji kimoja na kuwauwa raia watatu.