Colombo: Mabalozi wa nchi za Magharibi wajeruhiwa huko Sri Lanka | Habari za Ulimwengu | DW | 28.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Colombo: Mabalozi wa nchi za Magharibi wajeruhiwa huko Sri Lanka

Mabalozi wa Kijerumani, Kitaliana na kimarekani walijeruhiwa kidogo huko Sri Lanka katika shambulio lililofanywa na waasi wa Kitamil wa Tiger. Helikopta iliokuwa ikiwachukuwa mabalozi hao ilishambuliwa ilipokuwa inatua katika mji wa mashariki wa Batticaloa. Wengine waliojeruhiwa katika shambulio hilo ni polisi saba na wafanya kazi wawili wa jeshi la wanahewa. Helikopta hiyo pia ilikuwa ikiwachukuwa mabalozi wa Kanada, Ufaransa, Japan na Uengereza. Kikundi hicho kilikuwa kinakwenda kuutembelea mradi wa maendeleo. Wapiganaji wa Kitamil wa Tigers walisema wanasikitishwa kwamba mabalozi hao walijeruhiwa, lakini walililaumu jeshi la Sri Lanka kwa kuwapeleka katika eneo la michafuko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com