Colin Powell amuunga mkono Obama | Habari za Ulimwengu | DW | 19.10.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Colin Powell amuunga mkono Obama

Washington:

Waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje wa Marekani katika utawala wa Rais wa sasa George W.Bush, Colin Powell ametangaza kumuunga mkono mgombea wa Wademocrats katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo Barack Obama. Colin Powell alisema wote wawili Obama na mpinzani wake mgombea wa Raepublican John MacCain wanasifa za kuweza kuwa Amiri Jeshi mkuu, lakini Obama anaweza kuyashughulikia vizuri zaidi masuala ya uchumi na kuboresha sifa na msimamo wa Marekani duniani. Bw Powell alielezea kusikitishwa kwake na matamshi anayotumia Bw McCain katika kampeni yake pamoja na uteuzi wake wa Gavana wa Alaska Sarah Palin kuwa mgombea mwenza wa Warepublican. Alisema haamini Palin anauwezo wa kushika wadhifa wa Urais ikilazimika.Uchaguzi wa Rais nchini Marekani utafanyika tarehe 4 mwezi ujao wa Novemba

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com