1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chuki yamuondoa Borislav wa Bulgaria.

Lilian Mtono
15 Oktoba 2019

Rais wa shirikisho la soka la Bulgaria Borislav Mihaylov amejiuzulu kufuatia matamshi ya chuki yaliyotolewa na mashabiki wakati wa mechi ya kufuzu michuano ya Euro 2020 mjini Sofia.

https://p.dw.com/p/3RKnm
Bulgarien - England - Qualifikation zur UEFA Euro 2020 - Gruppe A - Vasil Levski National Stadium
Picha: picture-alliance/AP Photo/V. Ghirda

Waziri Mkuu wa Bulgaria Boyko Borissov aawali alimtaka rais huyo wa shirikisho la soka ajiuzulu, kufuatia matamshi ya kibaguzi dhidi ya wachezaji weusi wa kikosi cha England. Kwenye mechi hiyo, England iliwacharaza Bulgaria kwa mabao 6-0.

Mechi hiyo ambayo ilisimamishwa mara mbili na al manusura isitishwe kutokana na baada ya  mashabiki wa Bulgaria kuanza kutoa matamshi yenye mrengo wa ubaguzi wa rangi huku wengine wakiwaiga tumbiri wakiwalenga wachezaji weusi wa England. Wengine walionekana wakipiga saluti za kinazi. 

Waziri huyo mkuu wa Bulgaria alisema rais wa shirikisho la soka nchini humo Borislav Mihaylov anatakiwa kuwajibika kufuatia tukio hilo lililosababisha aibu nchini humo.

"Ninamuomba Borislav kujiuzulu mara moja!" aliandika Borisov kwenye Facebook. "Haikubaliki kuihusisha Bulgaria...taifa linalowavumilia watu wa dini na makabila tofauti na ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni," alisema.

Waziri mkuu huyo alionesha kutoridhishwa na matokeo hayo mabaya dhidi ya Bulgaria akisema ni "matokeo ya aibu".

Amemuagiza waziri wa michezo Krasen Kalev kuondoa misaada yote ya kifedha hadi rais huyo atakapojiuzulu.

Wachezaji watatu wa England, Raheem Sterlin, Marcus Rashford na Tyrone ndio waliolengwa na matamshi hayo ya kibaguzi. Sterling aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter akiikaribisha hatua hiyo ya waziri mkuu wa Bulgaria.