China yatangaza siku tatu za maombolezi | Habari za Ulimwengu | DW | 18.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

China yatangaza siku tatu za maombolezi

-

BEIJING

China imetangaza siku tatu za maombolezi baada ya watu 32,000 kufariki kufuatia tetemeko baya la ardhi kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika kipindi cha miongo mitatu.Serikali ya China imetoa taarifa inayosema kwamba majengo yote ya kiserikali yatapeperusha bendera ya taifa nusu mlingoti kwa siku tatu.Hapo kesho nchi nzima itakaa kimya kwa muda wa dakika tatu kuadhimisha wiki moja tangu kupiga tetemeko hilo la ardhi lenye nguvu za 7.9 katika kipimo cha richta kwenye mkoa wa Sichuan.Mapema hii leo rais Hu Jintao alizishukuru nchi za kigeni zilizotoa misaada kwa nchi yake baada ya kukutana na wafanyikazi wa mashirika ya misaada katika jimbo hilo la Sichuan.Saa chache zilizopita jimbo hilo lilikumbwa na tetemeko jingine dogo lililokuwa na kipimo cha 6.0 katika vipimo vya richta.Bado wafanyikazi wa misaada kutoka nchi mbali mbali wako katika eneo hilo wakiendelea na shughuli za uokozi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com