1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

China yakanusha kuitumia Twitter kupenyeza ajenda zake

Mohammed Khelef
26 Aprili 2022

Kumeibuka hofu juu ya uhuru wa Twitter baada ya kutwaliwa na bilionea Elon Musk.

https://p.dw.com/p/4ARou
Logo von Twitter ist auf einem Smartphone
Picha: Jakub Porzycki/NurPhoto/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya China imekanusha shutuma kwamba itatumia ushawishi wake kwa kampuni ya kutengeneza gari zinazoendeshwa kwa umeme, Tesla, ili kuathiri maudhui yanayorushwa na mtandao wa kijamii wa Twitter wenye makao yake makuu nchini Marekani, siku moja baada ya mmiliki wa Tesla kuinunua Twitter kwa dola bilioni 44 taslimu.

Elon Musk, mzaliwa wa Afrika Kusini, alitangazwa hapo jana kuwa mmiliki rasmi wa kampuni ya Twitter, baada ya kuweka dau kubwa akisema anataka kuubadilisha mtandao huo wa kijamii kuwa na faida zaidi kuliko sasa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Wang Wenbin, alikuwa akijibu swali la waandishi wa habari hivi leo, baada ya hofu kuzuka juu ya uhuru wa Twitter baada ya kutwaliwa na bilionea huyo.

Takribani nusu ya gari za Tesla zilizouzwa kote ulimwenguni mwaka jana zilitengenezwa kwenye kiwanda chake cha Shanghai, nchini China.