1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yabadili mfumo wa kunyonga wahalifu

19 Juni 2007

China ikitiwa msukosuko kwa hukumu zake nyingi za vifo kwa wahalifu,imegeukia kufuta adhabu hizo kwa fidia kwa wahanga.

https://p.dw.com/p/CHkW

China ikijiandaa kwa michezo ya olimpik ya majira ya kiangazi ya mwaka ujao huku ikishinikizwa kupunguza idadi ya adhabu zake za vifo,imekuwa ikijaribu kuondoa hukumu za vifo na badala yake kutoa adhabu za vifungo vya maisha.

Hatahivyo, mtindo wake mpya unazusha pia malalamiko.

Mlolongo wa kesi katika mkoa wa kusini wa Guangdong ambako waliohukumiwa kunyongwa walipewa msamaha wa kunyongwa na badala yake walipe fedha kwa familia za waliouliwa ni mtindo uliozusha mashaka mapema mwaka huu.Mtindo kama huo umeripotiwa pia katika mkoa wa pwsani wa Shandong na Zhejiang.

Kufichuka kwa taarifa hizi, kumeibua mjadala motomoto katika majukwaa ya mtandao wa Internet kuhusu thamani ya maisha ya mwanadamu katika nchi inayokosolewa mara kwa mara kwa kuwanyonga watu kila mwaka kuliko nyengine yoyote duniani.

Wakati hatua zikipata kasi miaka ya karibuni kubadili mfumo wa adhabu za kifo nchini China, uchunguzi umebainsha kuwa machina wengi wanaendelea kuiona adhabu ya kifo ndio ngao barabara ya kuzuwia uhalifu.

Hali ya kufadhahika kutoajua ifanyeje serikali ya China, inabainishwa na kesi ya mama mzee Deng Rongfen, huko mkoani Guangdong.Kisa chake

kilioripotiwa na gazeti moja la huko mwezi Machi.

Mtoto pekee wa kiume wa mama huyo mzee ambae akimtegemea kwa mkate katika ukoo wa watu 5, alipigwa kisu na kufariki hapo Mei mwaka jana.Aliwagundua wafanyikazi 3 wakivunja nyumba yao ili kwiba.Wote wakapewa adhabu ya kifo.

Lakini, hata ikiwa haki imetekelezwa karatasini,hali ya ukoo wa Deng imesalia kuwa vile vile mbaya.Bibi Deng hana fedha au mbinu ya kuwapeleka wajukuu zake Kindergarten au hata kumsaidia mke wa marehemu kuwalea watoto wao.

Wakuu wa mahkama katika mkoa wa Dongguan wameutetea mtindo wao mpya wa kutoa msamaha wa kutowanyonga wahalifu kwa fedha .Wanadai msamaha huo hutolewa tu kwa ridhaa ya ukoo wa mhanga.wanatoa hoja kuwa ukosefu wa mfumo mmoja wa malipo ya fidia wanaolipwa jamaa wa mhanga alieuliwa waweza kusaidia kuwapunguzia jamaa hao shida.

Kiroja cha mambo kuhanikiza kisa hiki hadharani kwa njia ya kuripotiwa yabainika kuleta matokeo yasiokusudiwa:Kumechochea mjadala juu ya ukosefu wa usawa katika jamii nchini China kwa kubainisha ukosefu wa mapato sawa.

Hatua ya serikali kuu ya China yafaa kupongezwa kuwa Mahkama kuu zitakomesha mfumo wa miaka 25 ulioziachia mahkama za kimkoa kupitisha adhabu za kunyonga watu.Kuanzia sasa ni Mahkama kuu itakyokagua kesi za adhjabu za vifo.

Hatahivyo, mabingwa wa sheria wa China, wanaamini idadi ya watu wanaonyongwa nchini yaweza kufikia hadi 10.000 kwa mwaka, licha ya marekebisho hayo yaliofanywa.