1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na bidha za maziwa

26 Septemba 2008

Shirika la WHO ladai ulimwengu ujifunze kutoka kashfa ya maziwa nchini China.

https://p.dw.com/p/FPV6

Nchini China,kwanza yaligunduliwa madawa katika na nyama ya kuku na ya nguruwe.Halafu madawa ya kuua vijidudu vinavyoharibu mimea yakagunduliwa katika mboga na sasa kemikali ya "melamin" katika bidhaa za maziwa.Idadi ya kashfa zinazotokana na bidhaa za vyakula nchini China yadhihirika haimaliziki.Hali hii akiitambua zamani mjumbe wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) nchini China Bw.Hans Troedsson.

Rasmi imetangazwa ni watoto wachanga 3 tu waliofariki dunia kutokana na maziwa yaliochanganywa kemikali ya "Melamin" ili kuongeza protein ingawa vyombo vya habari vimeripoti vifo 4 .Katika kesi 12.000 za watoto walioambukizwa na wanaotibiwa mahospitalini nchini China,kiasi cha watoto100 hali zao ni taabani.Hatahivyo, tusitarajie idadi ya vifo hivyo kuongezeka mno.

Watoto hao 3 wamefariki kutokana na maumbukizo kwavile, walikawia kupelekwa hospitali kutibiwa.Watoto ambao wakati huu wako katika hospitali inayotibu magonjwa ya figo waweza kutibiwa barabara . Hii ni kwa muujibu Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa lilivyoarifu.Jorgen Schlundt-mkurugenzi wa shirika hilo anaehusika na vyakula amezungumzia pia bidhaa zinazotengezwa kwa maziwa na zinazosafirishwa ngambo na China.

Bidhaa zinazouzwa nje ni muhimu kutambuliwa iwapo hazina dhara za afya .Wahusika nchini China wameyachunguza makampuni na viwanda vyote vinavyosafirisha bidhaa nje.Katika viwanda 2 wamegundua ukosefu wa usafi.Wakaziarifu nchi 5 ambako bidhaa za viwanda hivyo zilisafirishwa bila kuwa na uhakika zilipokea mazao ya unga wa maziwa yenye kasoro.Isitoshe, nchi hizo zinapaswa kuchungua ni bidhaa gani zinapokea kutoka China.

Nchi zenyewe ni Gabun,Burundi,Yemen,Bangkladesh na Birima.Kwa jumla, taarifa za bidhaa za maziwa zisizo safi kutumiwa zimeustusha ulimwengu mzima.Kila pahala saasa ishara ndogo tu zinazobainisha kemikali hiyo ya Melamin huchunguzwa.

Hatahivyo, Bw.Jorgen Schlundt ameonya kutoeneza hofu na kihoro:Kemikali ya Melamin inakutikana katika vipaketi mbali mbali na huingia kidogo katika vyakula .Hii haina dhara.Hali inakuwa mbaya inapotuwama mno katika vyakula.Hapa tunazungumzia kipimo kinachovuka mara laki 1.Hapo tena ndio huwa hatari kwa afya na mgonjwa hubidi kutibiwa.Kwani, hupata maradhi ya mawe katika mafigo.

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) sasa linatupa macho mbele na linachunguza vipi kuepuka kashfa kama hii itaweza kuepukwa.Shauri linalotolewa kwa China ni kuwa, sio tu China inahitaji kuwa na sheria ili wazi kabisa na muongozo bali sheria na muongozo huo utumiwe barabara.

Na hili ndilo tatizo kuu kwa china -dola la chama kimoja lisilo na ukaguzi huru .

Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa laonya hatahivyo, kutoipiga mhuri China kuwa chanzo cha balaa lote.Kuweka utaratibu wa ukaguzi katika viwanda vikubwa vinavyotengeza vyakula si rahisi-asema Jorgen Schlundt kutoka Denmark.Na hakuna binadamau aliekamilika. Anaongeza:

"Tunaweza kuilinganisha China na nchi nyengine.1995 tulipatwa na balaa la maradhi ya kichaa cha ngombe BSE ambacho kilitapakaa kutoka nchi za umoja wa Ulaya hadi ulimwengu mzima. Muda mfupi baadae, tukakumbwa na kashfa ya sumu ya Dioxin nchini Ubelgiji.Lakini hatukusema wakati ule kuwa bidhaa zote zitokazo Ulaya zina sumu. Matatizo kama haya yapo pia katika nchi zilizoendelea na hata zile zinazoinukia.Sasa tuisaidie China kuimarisha na kukuza idara zake za kukabiliana na hali kama hizi.Lakini kudai kuwa matatizo yote yanayohusiana na vyakula vilivyoambukizwa chanzo chake ni China,si sahihi kabisa. "