1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China, Afrika zasaini makubaliano ya kibenki

Sudi Mnette
11 Septemba 2018

Benki 16 za Afrika ikiwemo RAWBANK, taasisi ya kwanza ya kibenki katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na Benki ya Maendeleo ya China wametia saini kuanzishwa kwa makubaliano ya muungano wa kibenki.

https://p.dw.com/p/34f5w
Präsident von Mali Ibrahim Boubacar Keita
Picha: Getty Images/AFP/R. Pilipey

Hayo yanafanyika katika kipindi hiki ambacho mradi wa ujenzi wa reli na mahusiano mengine ya kibiashara yakizusha hofu ya deni kubwa na nia ya China ya kulipunguzia nguvu bara hilo kisiasa katika usimamizi wa rasilimali zake.

Hivi punde RAWBANK, imechaguliwa kuwa mwanachama katika ushirikiano huo, ikiwa na jukumu kubwa la kuongoza sekta ya kibenki nchini Congo, sambamba na benki nyingine za kimataifa, na za Kiafrika. Makubaliano hayo sasa yanathibitisha uanzishwaji wa ushirikiano wa kifedha kati ya Afrika na China. Kwa mujibu wa Rais Xi Jinping, China ina lengo la kuimarisha uhusiano wake na Afrika kwa kile alichokitaja "Mipango ya kanuni 10 ya ushirikiano" kwa lengo la kuendeleza ushirikiano.

Malengo ya muungano wa kibenki

Senegal Xi Jinping auf Staatsbesuch
Marais Xi Jinping wa China na Macky Sall ya SenegalPicha: Reuters/M. McAllister

Kuzingatia upungufu ulipo katika sekta mbalimbali mkutano huo umeamua kuwa kuna umuhimu kutoa fedha kwa mataifa ya Afrika zingatio likiwa ni kuendeleza viwanda, uunganishaji wa miundombinu na kupunguza umasikini pamoja na huo ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za fedha za Kichina na nchi za Afrika.

Wakati hayo yakifikiwa, wimbi la miradi ya ujenzi wa reli na ushirikiano mwingine wa kibiashara bainia ya pande hizo mbili yaani Afrika na China, limezusha hofu kuhusu deni pamoja na tamaa ya serikali ya China ya kutaka kupunguza kisiasa usawa kwa mataifa ya Afrika ili ijijengee uwezo katika uamuzi mbalimbali. Utafiti mpya wa asasi ya Kimarekani iitwayo AidData ya chuo cha William & Mary ya huko Virginia imefanya utafiti katika miradi 3,485 katika mataifa 138 katika eneo la Asia, Afrika, Amerika ya Kusini na Mashariki ya Kati.

Pamoja na kugusia miradi ya mataifa mengine lakini ripoti hiyo ilijikita kwa China. Matokeo jumla yanaonesha kumekuwa na maswali magumu katika miradi hiyo. Baadhi ya dokezo za utafiti wa ripoti hiyo zilionesha miradi ya China kugubikwa na rushwa na uharibifu wa kimazingira. Viongozi barani Afrika, Asia Kusini na maeneo mengine wameiukubali kwa shangwe miradi ya China ukiwemo ule mkubwa wa ujenzi wa reli na barabara, ambao upo katika sera za mambo ya nje ya Rais Jinping, lakini wamekuwa wakilalamika kuhusu gharama kubwa.

Baadhi ya serikali ikiwemo ya Nepal, Sri Lanka na Thailand wameachana na miradi hiyo kutokana na ughali wake au wakati mwingine malalamiko ya kazi chache sana zinakwenda kwa makampuni ya ndani ya mataifa husika. Nchini Kenya rais Uhuru Kenyatta anakabiliwa na maandamano na migomo kutokana na nyiongeza ya kodi ya asilimia 16 ya mafuta ikielezwa tozo hilo lina lengo la kulipa gharama za miradi ya ujenzi.

Mwandishi: Sudi Mnette APE/RAWBANK
Mhariri: Josephat Charo