CHICAGO:Mgomo wa wafanyikazi wa GM wapatiwa ufumbuzi | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CHICAGO:Mgomo wa wafanyikazi wa GM wapatiwa ufumbuzi

Chama cha muungano wa wafanyikazi wa makampuni ya magari kimefikia makubaliano na kampuni ya magari ya General Motors ya Marekani kumaliza mgomo wa wafanyikazi uliodumu kwa siku mbili.Chama hicho kinachotetea maslahi ya wafanyikazi hao kimesema kitawashawishi wafanyikazi wa kampuni hiyo kurudi kazini mara moja.Hata hivyo makubaliano yaliyofikiwa yatabidi kuangaliwa upya na kuidhinishwa na wakuu wa chama hicho cha wafanyikazi na hatimaye kupitishwa na mahakama.

Wafanyikazi hao waligoma kufanya kazi kutokana na kushindwa kwa kampuni ya GM kuwahakikishia juu ya bidhaa za siku za usoni na vitega uchumi katika kampuni za Marekani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com