Chelsea yamsaini Abdul Rahman Baba kutoka Augsburg | Michezo | DW | 17.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Chelsea yamsaini Abdul Rahman Baba kutoka Augsburg

Chelsea imemsaini beki wa kushoto Abdul Rahman Baba kutoka klabu ya FC Augsburg ya Ujerumani. Chelsea na Augsburg zimethibitisha kukamilisha usajili wa beki huyo raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 21 kupitia tovuti zao

Usajili huo umefanyika kujaza nafasi ya beki wa kushoto baada ya Mbrazil Luis Filipe kurudi katika timu yake ya zamani ya Atletico Madrid nchini Uhispania

Mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho, amepongeza usajili huo akisema kuwa anaamini mlinzi huyo ataleta ushindani kwa Cesar Azpilicueta katika nafasi ya beki wa kushoto.

Rahman amekuwa katika klabu ya Augsburg kwa miezi 12 ambako alisajiliwa akitokea timu ya SpVgg Greuther Fürth mnamo Agosti mwaka 2014.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Sessanga