Chelsea kuanza kampeni ya kutetea taji | Michezo | DW | 19.09.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Chelsea kuanza kampeni ya kutetea taji

Siku ya pili yamichezo ya EUFAChampions League,inazikutanisha timu za makundi ya E,F,G, na H,ambapo mabingwa watetezi wa taji hilo Chelsea ya mjini London itakuwa uwanjani kupimana nguvu na Juventus Turin ya Italia.

Chelsea's players celebrate after their FA Cup final soccer match against Liverpool at Wembley Stadium in London, May 5, 2012. REUTERS/Eddie Keogh (BRITAIN - Tags: SPORT SOCCER)

FC Chelsea mabingwa wa mwaka 2012 wa Champions League

Huko mjini Bayern makamu bingwa wa Bundesliga , Bayern Munich inatiana kifuani na Valencia ya Uhispania. Huu utakuwa mchezo kama wa marudio ya fainali ya mwaka 2001 ya Champions League kati ya timu hizo ambapo Bayern Munich iliibuka kidedea kwa kuishinda Valencia kwa mikwaju ya Penalti.

Manchester United inapata somo kwa yaliyoikuta msimu uliopita baada ya kuyaaga mashindano hayo katika duru ya kwanza:

Mabingwa watetezi Chelsea London itawawia vigumu zaidi kushinda taji la Champions League la msimu huu wa 2012-13 kuliko ilivyofanya msimu uliopita, amesema hivyo kocha wa timu hiyo Roberto Di Matteo katika mkesha wa mchezo wake wa kwanza nyumbani dhidi ya Juventus Turin .

Chelsea's interim head coach Roberto Di Matteo blows his whistle during a Champions League final training session at the club's training ground in Stoke D'Abernon, England, Tuesday, May 15, 2012. Chelsea are due to play Bayern Munich in the final of the Champions League in Germany on Saturday. (Foto:Matt Dunham/AP/dapd).

Kocha wa FC Chelsea Roberto Di Matteo

Watoto hao wa mjini London pia wamewekwa pamoja katika kundi lao la E, na Shakhtar Donetsk mabingwa wa Ukraine na Nordsjaelland ikiwa ni mabingwa wa Denmark.

Di Matteo amekiri kuwa timu zilizoingia katika Champions League msimu huu ni ngumu mno. Mashindano haya msimu huu ni magumu kuliko msimu uliopita, amesema Di Matteo.Chelsea ilipata taabu kwa kiasi kikubwa kuweza kushinda taji hilo msimu uliopita , kwa kufanikiwa kubadilisha kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Napoli ya Italia katika duru ya timu 16, na kuwaondoa njiani Barcelona katika nusu fainali , kabla ya kuishinda Bayern Munich katika fainali nyumbani kwa Bayern.

Bayern: yaliyopita si ndwele

Nayo Bayern Munich itataka kuthibitisha kuwa imefuta majonzi ya kushindwa katika fainali hiyo na Chelsea wakati wakiwakaribisha Valencia ya Uhispania katika uwanja wake wa Allianz Arena mjini Munich.

Kocha Jupp Heynckes anaweza kuwatumia mawinga Arjen Robben na Frank Ribery leo , ambao walikuwa majeruhi, na kushindwa kuwamo kikosini , katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mainz 05 katika mchezo wa Bundesliga mwishoni mwa juma.

Bayern Munich's Arjen Robben celebrates a goal against Real Madrid during their Champions League semi-final second leg soccer match at Santiago Bernabeu stadium in Madrid, April 25, 2012. REUTERS/Felix Ordonez (SPAIN - Tags: SPORT SOCCER)

Arjen Robben FC Bayern München itaweza kumtumia leo

Kocha wa Valencia , Mauricio Pellegrino ambaye alikuwa kikosini wakati Bayern Munich ilipoishinda timu hiyo katika fainali ya Champions League mwaka 2001, leo atakaa katika benchi la ufundi akikiongoza kikosi hicho ambacho kimepata ushindi wake wa kwanza katika ligi ya Uhispania , La Liga dhidi ya Celta Vigo wiki iliyopita.

Kocha Pellegrino amesema , kikosi chake hakipaswi kuiogopa Bayern.

Mapambano mengine jioni ya leo ni kati ya Barcelona na Spartak Moscow , Celtic Glasgow inakwaana na Benfica ya Ureno katika kundi G , na Manchester United iko nyumbani kupimana nguvu na mabingwa wa Uturuki Galatasaray. Braga ya Ureno inawakaribisha CFR Cluj.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / dpae

Mhariri : Yusuf Saumu