1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chavez ashinda kura ya mabadiliko ya katiba

Aboubakary Jumaa Liongo/AFP16 Februari 2009

Rais Hugo Chavez wa Venezuela ameshinda katika kura ya kuifanyia mabadiliko katiba ya nchi hiyo, iliyofanyika hapo jana.

https://p.dw.com/p/Gv4d
Rais Hugo ChavezPicha: DW

Mabadiliko hayo yanataka kuondolewa kwa kipengee cha ukomo wa mtu kugombea urais pamoja na ugavana wa majimbo.

Matokeo hayo sasa yanamfanya Rais Chavez kuweza kuwania tena urais pindi atakapomaliza kipindi chake cha miaka kumi mwaka 2013.


Tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa asilimia 54.4 ya watu waliyopiga kura hiyo wamekubaliana na hatua ya kuifanyia mabadiliko katiba ya nchi hiyo, huku asilimia 45.6 wakikataa.


Rais Chavez ambaye ni mfuasi wa siasa za kisoshalisti sasa anaweza kuongoza kwa muda wowote anaotaka ili mradi ashinde katika uchaguzi.


Akiwahutubia maelfu kwa maelfu ya wafuasi watu kwenye makaazi yake, Rais Chavez, huku akiwa kavaa shati jekundu kama kawaida yake alipunga ngumi angani na kupaza sauti akisema ''Leo tumezaliwa upya kutoka katika mikono yenu, wadumu wananchi wa Venezuela, yadumu mapinduzi, udumu usoshalisti´´

Hotuba yake hiyo hata hivyo ilikuwa tofauti na nyingine anapotoa kushangilia ushindi ambapo huelezea sera na mikakati mipya.


Katika hotuba hiyo aliwaambia wafuasi wake kuwa iwapo wataimarisha mafanikio waliyoyapata, basi kwa kuanzia mwakani watakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kufungua mustakbali mpya na kwamba kumchagua yeye ni kuchagua maajaliwa ya watoto wao.


Wafuasi wake huku wakipunga bendera za nchi hiyo walimshangilia wakisema ´´Heh-ho Chavez´´ yaani Chavez aondoki.


Upande wa upinzani ulikubali kushindwa katika kura hiyo, ushindi ambao ni wa kiwango kikubwa kuliko ilivyokuwa ikitegemewa kutokana na kura za maoni zilizompa nafasi ya ushindi mdogo Chavez.


Kiongozi wa upinzani Leopoldo Lopez alisema Goliati ameshinda akimfananisha Chavez na Goliati ambaye anasimuliwa katika bibilia jinsi alivyopambana na Daudi aliyekuwa na mawe matano tu,yeye akiwa na silaha kubwa kama mkuki na ngao.


Mmoja wa wabunge wa upinzani nchini humo akizungumzia zaidi juu ya matokeo hayo alisema ´´Hatuamini kama uchaguzi huu ulifanyika katika mazingira ya kidemokrasia, lakini haya ndiyo matakwa ya wananchi wa Venezuela, tunawaheshimu watu wetu, tunaheshimu taasisi zetu, tunaimarisha demokrasia nchini Venezuela, kwahiyo ni lazima tukubali matokeo´´


Mjini Havana Rais wa zamani wa Cuba Fidel Castro amempogeza Rais Chavez kwa ushindi huo.Chavez amekuwa akimuita Castro kuwa ni baba yake kisiasa na alimjibu kwa kumuambia ushindi huo ni ushindi wake na watu wa Cuba pamoja na wananchi wa Latin Amerika.


Kiasi cha watu millioni 11 kati ya wakaazi millioni 17 wa nchi hiyo walipiga kura katika uchaguzi huo ambapo zaidi ya waangalizi 100 wa kimataifa walikuwa nchini humo kuufuatilia.


Rais Chavez alianza kujiingiza katika siasa mwaka 1992 wakati alipokuwa afisa kijana wa kikosi cha mianvuli aliposhindwa katika jaribio la mapinduzi ya kijeshi, ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka mwili