champions League | Michezo | DW | 26.11.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

champions League

Werder Bremen zamu yake leo

default

Miroslav Klose akisherehekea ushindi.

Baada ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich , jana kukata tiketi ya duru ijayo ya kutoana ya Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa kuikandika Steua Bucharest kwa mabao 3-0,leo ni zamu ya timu nyengine ya Ujerumani kutamba uwanjani:Werder Dremen inayocheza katika kundi B jioni hii na Famagusta ya Cyprus.Sporting Lisbon ya Ureno inaikaribisha FC Barcelona,viongozi wa Ligi ya Spain wakati huu.Liverpool ya Uingereza iko nyumbani ikicheza na Olympique Marseille wakati Atletico Madrid ina miadi na PSV Eindhoven.

Vigogo vikubwa kama Chelsea ya Uingereza,Inter Milan ya Itali na FC Liverpool leo zitapania kweli kujiunga na FC Barcelona ambayo kwa kweli imeshaingia duru ijayo ya kutoana ya timu 16. Werder Bremen ya Ujerumani,haitakuwa na kibarua kikubwa sana mbele ya Famagusta ingawa katika Bundesliga,Brtemen ililazwa jumapili iliopita na mahasimu wao wa kaskazini Hamburg 2:1.

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich walitamba jana wazi wazi kwa warumania Steua Bucharest kwa mabao 3:0. mabao 2 ya kipindi cha pili aliopachika jogoo lao Miroslav Klose na bao jengine la kichwa alilotia mtaliana luca Toni yalitosha kupiga msumari wa mwisho katika jeneza la Bucharest katika Champions League.

Ushindi wa Munich wa kuingia duru ijayo ameueleza Luca toni unatokana na majogoo 3 wa munich:Franc Ribery,Miroslav Klose na yeye mwenyewe Luca Toni."Kwani, alisema wao 3 wanafahamiana sana.

Bayern Munich sasa wako nafasi ya 3 katika ngazi ya Bundesliga na katika Champions League bado hawajashindwa. kocha wao Jurgen Klinsmann amefurahishwa na mchezo wa timu yake dhidi ya steau bucharest ambao wanaburura sasa mkia wa kundi lao.Kocha wa steua Bucharest Dorinel Munteanu alinukuliwa kusema,

"Tumefanya madhambi mengi na humudu kufanya hivyo ukicheza na Bayern Munich."

Licha ya kutamba kwa Munich wakati huu imezongwa na mashaka kuhusu mchezaji wake mmoja ambae hayumo katika kikosi cha washambulizi 3 aliowataja Luca Toni:Lukas Podolski. FC Cologne, klabu ya zamani ya Podolski, imethibitisha jana kwamba wana mipango ya kumrudisha mtoto wao Podolski nyumbani Cologne kutoka Bayern munich. Rais wa FC cologne,Wolfgang Overath na Meneja Michael Meier wamearifu kwamba FC Cologne wamezungumza na pande husika na sasa wanasubiri ishara kutoka Munich juu ya siku za usoni za stadi huyo.

Podolski mwenye umri wa miaka 23,aliachamkono Cologne kujiunga na Bayern Munich 2006 kwa kitita cha dala milioni 7.7 kwa mkataba wa hadi 2010.Hivi sasa lakini haridhiki kuachwa ubaoni tu akisota wakati akina Luca Toni,Riberry na Klose wanatamba.

Kesho ni zamu ya kombe la UEFA-kombe la shirikisho la dimba la Ulaya.Chalke klabu nyengine ya Bundeskiga, itakuwa uwanjani kupimana nguvu na Manchester City ya uingereza.Katika kundi hili A, Paris St.Germain ya Ufaransa ina miadi na Racing Santander ya Spian.

Stuttgart pia kutoka Ujerumani na inayopepesuka katika Bundesliga -hali iliopelekea kumtimua kocha wake Armin Veh mwishoni mwa wiki, itachuana kesho na Sampdoria ya Itali.Hamburg iliotamba mbele ya Werder bremen jumapili iliopita ikiongozwa na kocha wake mholanzi wana miadi na wadachi Ajax Amsterdam.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com