1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League: Real Madrid na Napoli zatinga Robo fainali

16 Machi 2023

Real Madrid wamefuzu kuingia hatua ya robo Fainali baada ya kuicharaza Liverpool bao 1-0 katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

https://p.dw.com/p/4OkmD
Champions League | Real Madrid vs FC Liverpool
Picha: Manuel Reino Berengui/DeFodi Images/picture alliance

Bao hilo la Madrid lilitiwa nyavuni na mchezaji mahiri na mshindi wa tuzo ya Ballon d´Or Karim Benzema katika dakika 78. Katika mechi nyingine, Napoli wamefuzu kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika historia yao baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt ya Ujerumani.

Lakini kabla hata ya mechi hiyo kuanza, kulishuhudiwa vurugu za mashabiki wa timu hizo mbili mjini Napoli.

Kwa sasa timu nane zitakazoshiriki robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zimebainika rasmi. Washiriki wanasubiri kufahamu watapangwa kukutana na timu gani katika droo itakayofanyika kesho Ijumaa mjini Nyon, nchini Uswisi.