Chama tawala Chad chashinda wingi wa viti bungeni
12 Januari 2025Chama tawala nchini Chad kimeshinda theluthi mbili ya viti katika uchaguzi wa wabungeuliofanyika mwezi uliopita kulingana na matokeo ya muda yaliyotolewa leo. Matokeo ya uchaguzi huo ambao kwa kiasi kikubwa ulisusiwa na upinzani, yanaimarisha utawala wa Rais Mahamat Idriss Deby madarakani.
Mamlaka ya uchaguzi imetangaza kuwa chama cha Deby cha Patriotic Salvation Movement, kimejizolea jumla ya viti 124 kati ya 188 katika bunge la kitaifa.
Uchaguzi huo ambao ulijumuisha chaguzi za manispaa na mikoa, ulisusiwa na chama cha kiongozi wa upinzani Succes Masra pamoja na vyama vingine kadha, vikisema ulikosa uwazi.
Deby alishinda urais katika uchaguzi mwingine iliozozaniwa mwezi Mei, miaka mitatu baada ya kujitangaza kuwa kiongozi wa muda wakati waasi walipomuua baba yake kwenye uwanja wa vita.