1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha ZANU-PF kimewafuta kazi wabunge 11 Zimbabwe

19 Januari 2018

Baadhi ya wabunge waliokumbwa na hatua hiyo walikuwa ni mawaziri katika serikali iliyokuwa ya Mugabe.

https://p.dw.com/p/2r8UN
Simbabwe Parlament | Amtsenthebungsverfahren Robert Mugabe
Picha: Reuters/A. Ufumeli

Chama tawala nchini Zimbabwe ZANU-PF  kimetangaza kuwafukuza ubunge,  wabunge  wake 11, washirika wa rais wazamani Robert Mugabe.

Haya yanajiri  mnamo wakati rais Emerson Mnangagwa akiendelea kuchukua hatua dhidi ya wale waliokuwa wakimuunga mkono Mugabe pamoja na mkewe Grace. Mnangagwa alishika madaraka Novemba mwaka jana  baada ya Robert Mugabe aliye na  umri wa miaka 93 kulazimishwa kujiuzulu baada ya jeshi kuchukua mamlaka.  

Naibu Spika katika bunge la  Zimbabwe  Mabel Chinomona amesema chama cha ZANU-PF kimeliarifu bunge kuwa wabunge hao kwa sasa hawawakilishi masilahi ya chama hicho. Baadhi ya wabunge waliokumbwa na hatua hiyo walikuwa ni mawaziri katika serikali iliyokuwa ya Mugabe.

Desemba mwaka jana chama cha ZANU PF kilitangaza kufuta uwakilishi wa wabunge watano washirika wa Mugabe  akiwemo Jonathan Moyo mmoja wa wanasiasa waliokuwa katika kundi lillokuwa likimuunga mkono  Grace Mugabe.