Chama cha rais wa Sri Lanka kinaelekea kupata ushindi
15 Novemba 2024Matokeo ya awali katika uchaguzi wa mapema wa bungenchini Sri Lanka yanaonyesha kwamba chama cha rais mpya Anura Kumara Dissanayake kinaelekea kupata ushindi wa kishindo.
Huku zaidi ya nusu ya kura katika uchaguzi wa bunge uliofanyika jana zikiwa zimehesabiwa, chama chake cha National People's Power NPP kilikuwa kikiongoza kwa asilimia 63 ya kura.
Kulingana na matokeo ya awali kutoka kwa tume ya uchaguzi, chama cha NPP ambacho kilikuwa na vitu vitatu pekee katika bunge lililomaliza muda wake, kwa sasa kinaongoza katika karibu kila jimbo katika bunge lenye viti 225.
Dissanayake alichukua mamlaka katikauchaguzi wa rais wa Septembakwa ahadi ya kupambana na ufisadi na kurejesha mali zilizoibwa, miaka miwili baada ya kuzorota kwa uchumi wakati rais Gotabaya Rajapaksa alipoondolewa madarakani.