1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha rais Bakiyev chaongoza katika matokeo ya uchaguzi

17 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CchR

Chama cha Ak Zhol cha rais wa Kyrgyzstan, Kurmanbek Bakiyev, kinajiandaa kushangilia ushindi mkubwa kufuatia uchaguzi wa bunge uliofanyika jana nchini humo.

Tume ya uchaguzi imesema chama tawala cha Ak Zhol kimeshinda asilimia 47, huku asilimia 70 ya kura zote zilizopigwa zikiwa zimehesabiwa.

Chama kingine kilichofaulu kupata zaidi ya asilimia 5 ya kura ili kiweze kuwakilishwa bungeni ni chama cha Ata Meken, kilichoshinda asilimia 9.7 ya kura.

Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi huo na mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema yameshuhudia visa vingi vya machafuko wakati wa zoezi zima la upigaji kura.