Chama cha rais Bakayev chashinda uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 17.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Chama cha rais Bakayev chashinda uchaguzi

Chama cha Ak Zhol cha rais wa Kyrgyzstan, Kurmanbek Bakiyev, kinajiandaa kushangilia ushindi mkubwa kufuatia uchaguzi wa bunge uliofanyika jana nchini humo.

Tume ya uchaguzi imesema chama tawala cha Ak Zhol kimeshinda asilimia 47, huku asilimia 70 ya kura zote zilizopigwa zikiwa zimehesabiwa.

Chama kingine kilichofaulu kupata zaidi ya asilimia 5 ya kura ili kiweze kuwakilishwa bungeni ni chama cha Ata Meken, kilichoshinda asilimia 9.7 ya kura.

Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi huo na mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema yameshuhudia visa vingi vya machafuko wakati wa zoezi zima la upigaji kura.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com