1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha CDU chakutana kuelekea uchaguzi wa kiongozi wao

Amina Mjahid
15 Januari 2021

Chama cha kihafidhina cha Kansela wa Ujerumani Angela Merkel CDU kinatarajiwa kuanza mkutano wake kuelekea kura muhimu ya kumchagua kiongozi wa chama hicho itakayofanyika tarehe (16.01.2021)

https://p.dw.com/p/3nxu8
Kanzlerin Merkel vor CDU-Logo
Picha: picture-alliance/AP/M. Probst

Kura hiyo ni hatua muhimu kuelekea kumchagua mrithi wa Merkel. Kufikia sasa haijabainika ni nani aliye kifua mbele katika kinyang'anyiro cha kuwania uongozi wa chama hicho.

Kuna wagombea watatu, Armin Laschet ambaye ni waziri mkuu wa jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya watu Ujerumani North Rhine-Westphalia, Wakili Friedrich Merz na mtaalam wa sera za kigeni Norbert Röttgen.

Laschet anaweka msisitizo zaidi katika haki za kijamii na usalama wa ndani.

"Je, chama chetu kinaiwakilisha jamii, jawabu ni hapana. Tukifanikiwa kuwavutia wahamiaji basi hapo tutakuwa na nafasi ya kusalia kuwa chama cha watu."

Kura hiyo inakuja katika mwaka muhimu sana kwa Ujerumani kwani uchaguzi wa kitaifa unatarajiwa kufanyika mwezi Septemba.

Merkel amepanga kustaafu kutoka kwenye siasa mwishoni mwa muhula wake huu ambao ni wa nne.