Chalsea yatoka sare na Juventus Champions League | Michezo | DW | 20.09.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Chalsea yatoka sare na Juventus Champions League

Katika safari ya kuwania kombe la vilabu bingwa barabi ulaya-Champions League, mabingwa watetezi Chelsea wameanza mbio hizo Jumatano (19.9.2012) kwa kutoka sare ya bao 2-2 katika mchezo wake na klabu ya Juventus.

Chelsea player Frank Lampard lifts the Champions League trophy as he celebrates with his teammates, during a parade in London, Sunday, May 20, 2012. Chelsea's Didier Drogba scored the decisive penalty in the shootout as Chelsea beat Bayern Munich to win the Champions League final in Munich, Germany after a dramatic 1-1 draw on Saturday, May 19. (Foto:Lefteris Pitarakis/AP/dapd).

Champions League Pokal Chelsea feiert in London

Kiungo wa kati wa wa Chelsea Mbrazili Oscar ndiye aliyeipatia klabu yake mabao yote mawili. Ikiwa ni mara yake ya kwanza kabisa kwao kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 kushiriki ligi hiyo, Oscar aliwaonyesha mashabiki kwa nini Chelsea iliamua kupoteza kitita cha paundi za Uingereza milioni 25 kumsajili kwa kushinda mara mbili katika dakika tatu za mwanzo dimbani Stamford Brigde.

Mbingwa wa Champions League, Chelsea waliposheherekea ushindi wa msimu uliopita jijini London.

Mbingwa wa Champions League, Chelsea waliposheherekea ushindi wa msimu uliopita jijini London.

Sare hiyo ya bao 2-2 iimewanyima raha mabingwa hao watetezi ambapo kocha wake Roberto Di Matteo amesema kuwa wamekosa fursa ya kuanza na ushindi. "Tumevunjika moyo na matokeo haya na kwa kiasi fulani tunajihisi kushindwa. Tulikuwa kwenye nafasi nzuri ya kutoka na ushindi lakini matokeo yake tumeambulia sare tu" anasema Di Matteo.

Kwa upande wao Juventus waliweza kuwanyanyua mashabiki wao vitini dakika 10 baada ya kuingizwa uwanjani Fabio Quagliarella ambaye aliipatia bao la pili timu hiyo.

Nayo klabu ya soka ya Barcelona ya Uhispania imeweza kuonyesha ubabe dhidi ya Spartak Moscow baada ya kuipa kipigo cha bao 3-2. Shukrani za pekee zinakwenda kwake Lionel Mersi ambaye alionyesha juhudi kubwa na kufanikiwa kuipatia ushindi timu yake. Barcelona ndiyo kinara katika kundi G.

Bayern yaanza kwa ushindi

Kwa upande wa klabu ya Bayern Munich kutoka hapa Ujerumani mambo hayakuwa mabaya kwani imeweza kuibuka na ushindi dhidi ya Valencia katika mchezo wake wa kwanza wa taji hilo tangu iliposambaratishwa na Chelsea katika fainali zilizopita mwezi Mei mwaka huu kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Mchezo kati ya FC Bayern München na FC Valencia

Mchezo kati ya FC Bayern München na FC Valencia

Manchester United wana wa Sir Alex Ferguson wakiwa katika kundi H ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Galatasaray. ushindi huo unatajwa kama wa kichovu kwani Galatasaray ilionyesha mchezo ambao uliwatoa jasho watoto wa jijini Manchester.

Hata hivyo Sir Alex Ferguson aliaambia wale wanaoona ushindi huo ni mwembamba kuwa kuanza msimu kwa pointi tatu ndilo jambo la msingi kwao hasa ukizingatia kilichowapata mwanzoni mwa msimu uliopita.

Gerard Piques kupata mtoto

Colombian singer, Shakira mama mtarajiwa wa mtoto wa Gerard Piques wa klabu ya Barcelona

Shakira mama mtarajiwa wa mtoto wa Gerard Piques wa klabu ya Barcelona

Baada ya kujua yanayoendelea katika mbio za kuwania taji la Champion sasa tuangalie mambo yanavyokwenda katika maisha ya mastaa wa kabumbu duniani. Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya Pop kutoka Colombia, Shakira ametangaza kuwa na ujauzito wa mchezaji wa kimataifa kutoka Uhispania Gerard Piques.

Kimwana huyo wa Hips Dont lie amesema hiyo ni hatua muhimu na ya pkee katika ulimwengu wa mapenzi baina yake na Gerard na atasimamisha baadhi ya maonyesha kwa wiki kadhaa ili kujipa nafasi ya kupumzika. Huyo atakuwa mtoto wa knza kati ya wenza hao ambao Shakira ana miaka 35 na Gerard ambaye ni mchezaji wa klabu ya kandanda ya Barcelona ana miaka 25 ambao waliweka wazi mapenzi yao mwezi Machi mwaka huu.

Mwandishi: Stumai George/Reuters/AFP